28.6 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

SUNGURA WAWA ‘DILI’ KIGOMA

Na EDITHA KARLO-KIGOMA
ZAIDI ya wananchi 3000 mkoani Kigoma, wanatarajia kunufaika na ufugaji wa sungura kibiashara, ikiwa ni mkakati wa wananchi hao kujiunga katika kilimo biashara ili kuondokana na umasikini.

Meneja Kilimo Biashara wa Namaingo Business Agency, Pascla Stephano, ameyasema hayo kwenye mkutano wa viongozi wa taasisi hiyo na wafanyabiashara wadogo na wananchi wa Mkoa wa Kigoma ambao wamehamasika kujiunga kwenye shughuli za uzalishaji zinazosimamiwa na taasisi hiyo.

Stephano alisema Mkoa wa Kigoma unayo fursa kubwa ya kuwafanya wananchi wake wakatumia ardhi na rasilimali mbalimbali walizonazo kuzalisha kibiashara na kuboresha hali za maisha yao, lakini bado watu wengi hawajaiona fursa hiyo na kuendelea kulima kimazoea.

Alisema tayari baadhi ya wananchi hao wameanza kuonyesha namna ambayo wanaweza kuitumia fursa hiyo kwa kuanzisha ufugaji wa sungura kibiashara, mradi ambao kwa sasa una soko na faida kubwa kwa wanaofanya ufugaji huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Biubwa Ibrahim, alisema Watanzania wengi ni waoga katika kutumia fedha kujiajiri wenyewe na hivyo wengi wanawekeza fedha nyingi katika masomo ili wapate ajira serikalini na kwenye mashirika mbalimbali badala ya kudhamiria kujiajiri baada ya masomo yao.

Mkurugenzi huyo alisema kilimo ndiyo sekta inayoweza kutumika na kuwaondolea wananchi umasikini iwapo watafanya kilimo chao kuwa cha kibiashara.

Baadhi ya washiriki wa mkutano huo walisema kuwa mada na taarifa mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji zimewafungua macho wananachi na wajasiriamali wengi.

Mmoja wa washiriki wa semina hiyo, Amani Simba, alisema amegundua kuwa kilimo biashara na ufugaji vinayo nafasi kubwa katika kuwakomboa Watanzania wengi kiuchumi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles