26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SUMAYE: WANANCHI WANA HAKI YA KUMKOSOA RAIS

NA MWANDISHI WETU– GEITA


WANANCHI wana haki ya kumsema au kumkosoa Rais na serikali iliyopo madarakani, kwa sababu nafasi walizonazo viongozi hao ni mali ya wananchi wenyewe.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (Chadema), Frederick Sumaye, alisema hayo jana alipozungumza kwenye Kongamano la Vijana wa Chadema (Bavicha) lililofanyika mkoani Geita.

Sumaye alisema katika mfumo wa demokrasia, serikali huwekwa madarakani na wapiga kura kwa kutekeleza matakwa yao kwa kufuata katiba, sheria za nchi, taratibu na hata desturi.

“Hao walioiweka serikali madarakani (wananchi) ndio wakubwa na wana haki ya kuiuliza serikali yao, Rais wao na mwingine yeyote mwenye madaraka. Baadhi yao wana haki ya kutofautiana kimawazo na viongozi wao walioko madarakani ikiwa ni pamoja na Rais,” alisema.

Alisema kwa msingi huo kutoa maoni yaliyotofautiana na alichokisema kiongozi wa serikali akiwamo Rais mwenyewe si usaliti, uhaini, uchochezi wala kukosa adabu.

“Kuna watakaomsifia sana, kuna watakaotoa ushauri wa tofauti na kuna watakaopinga na kuwa na msimamo tofauti na Rais na serikali yake, makundi yote matatu ni sahihi, hakuna msaliti wala mchochezi… ni vema yawepo kwa afya ya demokrasia.

“Kama wewe ni kiongozi na hutaki kusikia yale yaliyo kinyume na msimamo wako basi usipende pia kuyasikia na yale yanayokusifia sana.

“Leo  vyama vya siasa vimezuia kufanya mikutano ya hadhara ili viwajulishe watu wavyotaka kuwajulisha. Bunge ambalo ndiyo hufanya kazi kwa niaba ya wananchi shughuli zao huzionyeshwi mubashara kama huko nyuma,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles