Na ELIUD NGONDO, MBEYA
WAZIRI Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Fredrick Sumaye, alisema nchi inashindwa kuendelea kwa sababu inaendeshwa kwa ushabiki wa kisiasa hata katika masuala yenye masilahi kwa Taifa.
Sumaye aliyasema hayo mwishoni mwa wiki kwenye kongamano la Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema (Bavicha) pamoja na Umoja wa Vijana wa
Vyuo Vikuu ambao ni wanachama wa chama hicho jijini Mbeya (Chaso).
Sumaye ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema mambo mengi yenye masilahi ya
Taifa hayapaswi kufanyiwa mzaha kwani yanaweza kuzusha madhara makubwa ambayo hayakutarajiwa.
Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, alitolea mfano suala la bajeti ya mwaka huu 2017/2017 kwamba inaonyesha wazi haina uhalisia wa maisha ya wananchi wa kipato cha chini ambao ni wengi.
Alisema bajeti hiyo ingechambuliwa vyema na chombo chenye uwakilishi wa wananchi yaani Bunge kama chombo huru, lakini katika miaka ya hivi karibuni limeingiliwa na Serikali ya chama tawala na hivyo kupoteza sifa yake ya kuwasimamia wananchi.
“Nchi kwa sasa inayumba na inashindwa kuendelea kutokana na kuendeshwa kishabiki, bajeti yetu ya mwaka uliopita fedha za miradi ya maendeleo
zilitolewa kwa asilimia 34 pekee na Serikali ilikiri, lakini sasa hivi wanakuja na bajeti kubwa zaidi ya hiyo ambayo haijatekelezwa na wabunge wa CCM wanashangilia,” alisema Sumaye na kuongeza: