30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Sumaye: Kuwania nafasi hii hakunishushii hadhi

Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kuu ya Chadema Kamati, Frederick Sumaye, akizungumza na wanachama wa chama hicho baada ya kurejesha fomu za kugombea nafasi yaUenyekiti wa Kanda ya Pwani katika Ofisi za kanda Dar es Salaam jana.
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kuu ya Chadema Kamati, Frederick Sumaye, akizungumza na wanachama wa chama hicho baada ya kurejesha fomu za kugombea nafasi yaUenyekiti wa Kanda ya Pwani katika Ofisi za kanda Dar es Salaam jana.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye amesema nafasi anayoiwania ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani haimshushii hadhi kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana mara baada ya kurudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo.

Juzi Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, Mwita Waitara na wanachama wenzake walimchukulia fomu Sumaye na baadaye wakamkabidhi nyumbani kwake Kiluvya mkoani Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kurudisha fomu hizo, mwanasiasa huyo mkongwe aliyejiunga na Chadema Agosti mwaka jana, alisema nafasi hiyo ni muhimu kwake kwa kuwa chama hicho kinahitaji kuimarishwa kuanzia ngazi ya chini.

“Kuwania kwangu nafasi hii hakunishushii hadhi bali kunanipandisha, kwa sababu chama chetu kinahitaji kuimarishwa kuanzia ngazi za chini hivyo ni nafasi muhimu sana… hatuwezi kuwa na kiwiliwili bila kuwa na miguu.

“Lazima kuwe na vyama viwili vikubwa na tuwe na chama kikubwa kitakachokuwa kinashindana na CCM si kuwe na chama kikubwa kimoja tu na hii habari ya kung’ang’ania chama kimoja haiwezi kukuza demokrasia,”alisema Sumaye.

Alisema kitendo cha wanachama hao kumchukulia fomu kinaonesha wazi kuwa anafaa kwa sababu wako wengi ndani ya chama ambao wangefanyiwa hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chadema, Jimbo la Ilala, Allen Mezoko ambaye ni mmoja wanachama waliomchukua fomu, alisema wamefanya hivyo kutokana na hali halisi ya kisiasa nchini.

“Kuna nguvu kubwa inatumika katika mfumo wa Serikali uliopo, hivyo kupitia Sumaye ambaye pia alikuwepo kwenye mfumo huo katika nafasi hii anayowania tutaweza kulisimamia jiji,”alisema.

Wanachama wengine waliojitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo ni pamoja na John Gunnita, Gango Kidera huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikiwaniwa na Thomas Nyahende, Said Kubenea na Adolf Mkono.

Nafasi ya mweka hazina inawaniwa na Makongoro Mahanga, Lucy Magereli na Frolence Kasilima.

Wanachama waliorudisha fomu jana ni pamoja na Sumaye, Kidera na Nyahende.

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mara baada ya Kamati Kuu ya chama kuketi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles