25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

SUMAYE KUONGOZA KANDA YA PWANI

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye jana alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani kwa kupata kura 74 kati ya kura 89 zilizopigwa ambapo mshindi wa pili aliambulia kura15. Hakuna kura iliyoharibika.

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Salum Mwalimu alisema katika nafasi ya Makamu mwenyekiti, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea alishinda kwa kupata kura 60 wakati nafasi ya Mweka Hazina, Ruth Mollel alichaguliwa kwa kura 50.

Akizungumza baada ya matokeo hayo, Sumaye alisema atafanya kazi kwa bidii na kuhakikisha katika uchaguzi mkuu ujao wanashinda vijiji, kata na majimbo yote tisa ya Dar es Salaam.

"Nimekuwa Waziri Mkuu kwa miaka 10 ningeweza kubaki CCM nikala pensheni zangu na huku sijafuata cheo bali nimekuja kubadilisha sura ya siasa katika nchi hii," alisema Sumaye.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles