27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SUMAYE: KATIBA MPYA SAWA NA MAKINIKIA

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

 

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM 

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema Katiba mpya imewekwa pembeni kwakuwa watawala hawataki madaraka yao yadhibitiwe kupitia sauti huru za wananchi ambazo ni Katiba.

Alisema mchakato wa Katiba mpya umeigharimu nchi na kupoteza fedha nyingi za walipa kodi, sawa na mchanga wa dhahabu uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi (makinikia).

Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, aliyasema hayo Dar es Salaam  juzi kwenye mahafali ya vijana wafuasi wa chama hicho wa vyuo vikuu (Chaso) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Alisema Katiba inayopendekezwa pamoja na mambo mengine, inayo maoni ya wananchi na ilipitishwa na Bunge lakini inaonekana si jambo la kipaumbele na wala haitashughulikiwa tena kwa sababu itawadhibiti watawala.

“Mchakato wa Katiba mpya umeigharimu nchi fedha nyingi za walipa kodi sawa na makinikia lakini imetupwa, leo tunazungumzia makinikia, najua Rais Dk. John Magufuli  amekwishasema yeye haambiwi la kufanya, lakini sisi tutaendelea kumkumbusha yale ambayo tunadhani ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu,” alisema Sumaye na kuongeza:

“Si jambo la kupuuzwa, kama ni la kupuuzwa basi awakamate wote waliohusika na uamuzi huo maana ni ubadhilifu unaofanana na ule wa makinikia,” alisema.

Aidha, sumaye alisema Chadema  pamoja na washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wataendelea kudai Katiba mpya hadi itakapopatikana.

Aidha, kiongozi huyo wa Chadema  alieleza kwamba Tanzania ina mfumo bandia wa vyama vingi, huku kukiwa na chama kimoja kilichovaa ngozi ya vyama vingine.

“Tuna mfumo wa chama kimoja kilichovaa ngozi ya vyama vingi, mfumo wa vyama vingi vya siasa ni lazima ufuate utawala wa sheria na unaolinda, unaoheshimu na kuitetea Katiba ya nchi ambayo watawala wameapa kuilinda wanapokabidhiwa madaraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles