SUMAYE AONYA CHUKI ZA KISIASA

0
600

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema kuwa taifa halina chuki za kidini ila kwa sasa zinazoendelea ni chuki za kisiasa jambo ambalo amesema ni hatari kwa ustawi wa nchi na watu wake.

Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam juzi, alipokuwa akizungumza katika futari iliyoandaliwa na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), ambapo alisema jambo hilo halifai kufumbiwa macho.

“Tunamshukuru Mungu chuki baina ya dini hazipo kuna chuki za kisiasa ambazo ni hatari sana, tusipozitibu taifa linaweza lisibaki salama na viongozi wa dini wanatakiwa kukemea kwa kuombea hali hii ili ikawe sawa,” alisema Sumaye.

Alisema kwa kuendekeza chuki za kisiasa ambazo hazina maana na hazitakiwi kufika katika hali mbaya kwani si kazi ya binadamu kuishi kwa kisasi.

Kwa upande wake Kubenea, aliwashukuru wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chadema na Chama cha Wananchi (CUF) kushirikiana nao katika mambo mbalimbali ikiwemo la kufuturu pamoja na kupanga maendeleo ya jimbo hilo.

Aliwahakikishia atafanya kazi kwa kushirikiano kwani uchaguzi umekwisha kinachohitajika ni kufanya kazi kwa pamoja ili kulijenga jimbo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here