26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Suma G kutoka na Hang Over Januari

sumaNA BADI MCHOMOLO, DAR ES SALAAM

MKALI wa muziki wa kundi la Hot Pot Family, Ismail Self ‘Suma G’, amesema Januari mwanzoni anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao unajulikana kwa jina la Hang Over.

Msanii huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wake wa ‘Muulize Meneja’, amedai kwamba kutokana na ushindani uliopo kwenye muziki kwa sasa, lazima ujipange ili kushindana nao.

“Mwaka 2016 nilitaka kuanza kwa kasi kwa kuwa nimejipanga ili kwenda sawa na ushindani uliopo kwa sasa.

“Kuanzia Januari mwakani nitaanza kwa kuachia wimbo wangu mpya ambao utajulikana kwa jina la ‘Hang Over’ ambao nimemshirikisha ‘Chibwa’ umefanywa kwenye studio za Home Recods, chini ya mtayarishaji Eldo Bway,” alisema Suma G.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles