23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Sukari yasakwa kila kona

Mwandishi Wetu -Dar es salaam

BEI ya sukari imezidi kupaa huku iliyopo ikiadimika na hata kuuzwa kwa bei za kificho mitaani.

Kutokana na hali hiyo katika maeneo mbalimbali nchi hasa katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Tanga huku ikiuzwa kwenye baadhi ya maduka kwa Sh 4000 hadi 5000 kwa kilo moja.

Akizungumza hali hiyo baadhi ya wananchi ambao walizungumza na MTANZANIA jana walisema kuwa kwa sasa ni lazima Serikali itoe kauli badala ya kutoa bei elelezi lakini bado bidhaa hiyi imeadimika na hata kuuzwa kwa bei ya juu.

Mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, Kassim Mohamed alisema kuwa jana amelazimika kununua kilo moja kwa Sh 4,000 badala ya Sh 2,600 iliyotangazwa na Serikali jambo ambalo sasa linawaumiza kutokana na ugumu wa maisha.

“Nimekwenda dukani leo (jana) nimenunua kilo moja Shiling 4,000 jamani hali ni mbaya sana kwetu, maisha yamekuwa magumu tunaomba Serikali itusaidie,” alisema 

Hata hivyo katika maeneo ya Mlimani City, Mwenge na Sinza bei bidhaa hiyo imekuwa haipatikani katika baadhi ya maduka jambo ambalo linawafanya wananchi waisake bidhaa hiyo kila eneo.

Mkoani Morogoro jana baadhi ya wananchi walionekana wakiwa wamepanga foleni katika maduka makubwa ya sukari wakisubiri bidhaa hiyo.

KAULI YA SERIKALI

Hata hivyo Serikali imesema kuwa janga la ugonjwa wa corona limesababisha kuchelewa kwa uingizwaji wa sukari licha ya vibali kutolewa mapema

Hayo yamesemwa jana jijini Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa,  wakati wa ziara yake ya siku mmoja ya kukagua viwanda vipya ambavyo vinatarajiwa kuanza uzalishaji.

Alisema kuwa licha ya serikali kutoa vibali kwa wakati lakini janga la corona limesababisha changamoto katika usafirishaji wa sukari kuja nchini.

“Licha ya kasoro hiyo lakini bado serikali tumejipanga kila sukari inapoingia tumehakikisha hakuna urasimu bandarini na kuhakikisha inatoka kwa wakati na kuweza kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya nchini,” alisema Bashungwa.

Aidha akiwa katika kiwanda cha kuzalisha mkaa kwa kutumia vumbi la mbao cha African Flame waziri huyo,  alisema kuwa nia ya serikali kuifanya Tanga ya viwanda bado ipo pale pale na ujio wa viwanda hivyo ni sehemu ya mikakati hiyo.

Alisema kuwa uwepo wa viwanda vya kuzalisha chokaa pamoja na mkaa vitaweza kuleta fursa ya ajira kwa wakati wa Tanga na kuweza kuinua uchumi wa mkoa huo pamoja na nchi kwa ujumla.

“Nivitake viwanda vyote nchini kuhakikisha vinaendekea na uzalishaji huku vikizingatia ushauri wa wataalamu wa Afya kwa kulinda wafanyakazi wao ambao ni wazalishaji wakuu,” alisema 

BODI YA SUKARI

Wiki iliyopita Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Sukari Tanzania (SBT), Profesa Kenneth Bengesi alisema kuwa sukari ipo ya kutosha isipokuwa kuna wafanyabiashara ambao si waadilifu wanaficha ili wauze kwa bei kubwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,460FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles