SUGU, MASONGA KUKATA RUFAA

0
685

Pendo Fundisha na Eliud Ngondo, Mbeya

Upande wa utetezi katika ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) na Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga unakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu ya miezi mitano waliyopewa.

Hatua hiyo imekuja muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, kuwahukumu washtakiwa hao kwenda jela miezi mitano ambapo Wakili wa washtakiwa hao Peter Kibatala amesema wanakusudia kukata rufaa hiyo mapema.

Awali, akisoma hukumu hiyo leo Jumatatu Februari 26, Hakimu Michael Mteite amesema mahakama imejiridhisha kwamba mashahidi watatu upande wa mashitaka kwamba walikua kwenye mkutano hivyo waliona na kusikia.

“Pia ushahidi wa sauti na kwamba washitakiwa walitamka maneno hayo hivyo mahakama inawahukumu kwenda jela miezi mitano bila faini,” amesema.

Baada ya kumaliza kusoma hukumu hiyo, Wakili Peter Kibatala aliiomba Mahakama kupunguza adhabu katika adhabu itakayotolewa kwa kuwa walishakaa ndani mwezi mmoja waliponyimwa dhamana na pia washtakiwa hao ni wadogo na wana familia zinazowategemea.

Sugu na Masonga kwa pamoja wanadaiwa kutoa lugha hiyo ya fedheha kwa Rais, katika mkutano katika mkutano wa hadhara kwenye shule ya Msingi Mwenge, jijini Mbeya, Desemba 30, mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here