31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Sugu ashambuliwa kwa mawe Mbeya

NA PENDO FUNDISHA, MBEYA

MGOMBEA ubunge Jimbo la Mbeya Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amejikuta katika wakati mgumu baada ya msafara wake kushambuliwa na mawe na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika vurugu hizo, watu wawili wamejeruhiwa akiwamo dereva aliyekuwa akimwendesha mgombea huyo aliyejulikana kwa jina moja la Gabi, maarufu kwa jina la DJ BBG, ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Vurugu hizo pia zilisababisha gari aliyokuwa amepanda mgombea huyo kupasuliwa kioo cha mbele.

Vurugu hizo zilisababisha mgombea huyo ahairishe kuwahutubia wakazi wa Kata ya Iziwa jijini Mbeya kwa muda, kutokana na kulazimika kuripoti kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa maelezo.

Tukio hilo la kushambuliwa kwa msafara huo, limetokea saa 11 za jioni katika Kata ya Ghana – njia kuu ya kuelekea Kata ya Iziwa ambako mgombea huyo alikuwa anakwenda kuomba kura kwa wananchi.

Wakati msafara huo ukiwa katika mwendo, ulifika katika eneo la Kata ya Ghana, ambako kulikuwa na mkutano wa CCM wa kumnadi mgombea udiwani, ndipo ghafla ulianza kushambuliwa kwa kurushiwa mawe.

“Wakati wafuasi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wao ngazi ya udiwani katika Kata ya Ghana, msafara wa sugu ulipita katikati ya mkutano huo, hivyo kushindwa kuvumilia na kuanza kurusha mawe huku wengine wakishikana kutaka kupigana,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Wakati mshikemshike huo ukiendelea, imeelezwa kuwa Sugu alitoa taarifa polisi kuomba msaada ambapo askari walifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kutuliza  vurugu hizo.

Baada ya polisi kuingilia kati, Sugu alikwenda kituoni na kuchukuliwa maelezo na baada ya hapo aliruhusiwa kuendelea na shughuli zake, lakini gari yake T 161 CPP Toyota Land Cruiser VX aliyokuwa akiitumia katika kampeni zake ilibaki polisi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles