Sugu ampagawisha Waziri Mkuu

0
4102

Na Mwandishi wetu 


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amempagawisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwa kuimba mbele yao.
Sugu ambaye pia ni msanii wa nyimbo muziki wa kughani, ameimba leo Jumatano Novemba 7, wakati wa uzinduzi wa Mkakati wa Mpango wa kujumuisha masuala ya Jinsia ndani ya Bunge, jijini hapa.
Mara baada ya kupewa kipaza sauti sugu alianza kuimba wimbo wake wa chini ya miaka 18 hali iliyomfanya mara kadhaa Waziri Mkuu kupiga makofi kuonyesha kufurahishwa na burudani ya Sugu.
Uzinduzi huo umehudhuriwa pia na Spika Job Ndugai, Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai na wabunge wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here