26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

SUGU AITAKA SERIKALI KUWALIPA WASTAAFU MAGEREZA

Elizabeth Hombo, Dodoma


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu (Chadema), ameitaka serikali itawalipa askari wa magereza waliostaafu na kukaa zaidi ya miaka miwili.

Sugu amesema hayo wakati akiuliza swali bungeni jijini Dodoma leo wakati wa kipindi cha maswali na majibu.

“Mheshimiwa Spika, askari magereza wanacheleweshewa mafao zaidi ya miaka miwili, serikali inawaangalia kwa jicho lipi askari hawa kwanini mnawafanyia hivi askari maana ni miaka miwili wanadhalilika,” alihoji Sugu.

Baada ya Sugu kuhoji swali hilo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema aliacha Sugu ahoji swali hilo kwa muda kwa sababu ana uzoefu na anachouliza.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji amesema
mkakati wa kwanza wa serikali ni kulipa michango yote ya madeni na tayari imeshalipwa.

Amesema pamoja na hilo, tayari mifuko yote ya jamii imeshaunganishwa ili kuhakikisha wastaafu wote walipwa mafao yao.
Kutokana hilo, amesema zaidi ya Sh bilioni 282 imeshalipwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,560FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles