25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Sugu agoma kusoma hotuba ya upinzani bungeni, Dk. Tulia aagiza isiingie kwenye ‘hansard’

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Chadema),  amegoma kusoma hotuba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2018/20 kwa madai kuwa imehaririwa kwa kiasi kikubwa.

Sugu amelazimika kuchukua uamuzi huo leo Alhamisi Aprili 18, bungeni jijini Dodoma, baada ya  Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson kumtaka asisome baadhi ya maeneo yaliyoko katika hotuba yake.

 Kwa mujibu wa Dk. Tulia, hotuba aliyotaka kusoma Sugu ilikuwa na mambo yaliyoondolewa baada ya kuonekana yanakiuka kanuni za kudumu za Bunge.

 Kabla ya Sugu kuchukua uamuzi huo, alianza kusoma hotuba kupitia katika kitabu alichokuwa nacho lakini baada ya muda mfupi tangu alipoanza kusoma, Dk Tulia alimtaka asiisome bali asome kupitia kitabu kipya cha hotuba yake ambacho wabunge wote walikuwa wamegawiwa.

 Kutokana na maelekezo hayo,Sugu alisema hawezi kufanya hivyo kwani kitabu kipya hakina maoni ya kambi yake na hivyo kulazimika kuondoka mbele ya Bunge na kurudi katika kiti chake.

Baada ya kusema hayo Naibu Spika aliruhusu mjadala wa bajeti hiyo uanze huku akisema hotuba ya Sugu isiingizwe katika kumbukumbu za Bunge kwa kuwa Sugu hakusema kama anataka iingizwe katika kumbukumbu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,695FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles