27.5 C
Dar es Salaam
Friday, July 1, 2022

Sudan yaanza kufuatilia mali zilizonyakuliwa na Bashir

KHARTOUM, SUDAN

MAJENGO ya thamani ya mabilioni yaliyokuwa yakimilikiwa na utawala wa zamani wa Rais Omar al-Bashir yamerudishwa mikononi mwa serikali huku hatua kabambe za kuendelea kufuatilia mali nyingine nyingi ikifanyika kote Sudan

Mamlaka za Sudan zimeanza kuyachukua majengo ya mabilioni ya dola yaliyomilikiwa kinyume cha sheria na utawala wa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Omar al-Bashir. 

Kamati ya kupambana na rushwa nchini humo iliyoanza kazi mwezi Desemba inaamini kupatikana kwa mali hizo ni mwanzo wa kazi kubwa inayofuata ya kuzirudisha mali nyingi zilizopo mikononi wa Bashir zilizopatikana kwa njia isiyokuwa sahihi.

Wataalamu wanasema itakuwa vigumu baadhi ya mali kupatikana. Msemaji wa kamati iliyopewa jukumu la kupambana na rushwa na kuuvunja utawala wa zamani nchini humo Salah Manaa amesema makadirio ya awali yameonesha kwamba majengo na mali nyingine zilizomilikiwa na utawala huo wa zamani, thamani yake ni kati ya dola bilioni 3.5 mpaka 4.

Manaa aliliambia shirika la habari la AFP kwamba kilichoguswa hadi sasa ni sehemu tu ya vingi inapohusika mali jumla iliyopatikana kwa njia haramu na kufichwa chini ya utawala huo wa al-Bashir.

Al-Bashir aliitawala Sudan kwa mkono wa chuma kwa miaka 30, lakini aliondolewa kwa nguvu madarakani mnamo Aprili mwaka 2019 na jeshi la taifa hilo baada ya kufanyika maandamano makubwa ya wananchi walioupinga utawala wake. 

Kamati hii mpya ya kukabiliana na rushwa na ufisadi nchini humo ilianza kazi mwezi Desemba mwaka jana na inawajibika mbele ya serikali ya kugawana madaraka kati ya raia na majenerali wa kijeshi iliyoundwa mnamo mwezi Agosti.

Kiongozi huyo wa zamani alishtakiwa na kuhukumiwa miaka miwili jela katika kesi mojawapo ya rushwa inayohusiana na umiliki wa fedha za kigeni kinyume cha sheria.

Ikiwa ni chini ya miezi sita tangu ilipoanza kazi kamati hiyo inazifuatilia kwa ukaribu mali za rais huyo wa zamani. 

Duru zimeeleza kwamba kamati hiyo ilipokea lundo la nyaraka zinazojaza malori matatu ambazo zote zitahitaji kupekuliwa na kuchunguzwa kwa makini.

Kufikia sasa wachunguzi wanaohusika wameshapata hoteli kadhaa, mashamba, maduka, ardhi za kilimo na mali nyinginezo katika mji mkuu Khartoum na miji mingine zilizokuwa zinamilikiwa na jamaa na wasaidizi wa kiongozi huyo wa zamani.

Msemaji wa kamati ya kukabiliana na rushwa Salah Manaa alisema watalaamu wakimataifa watapelekwa nchini Sudan kusaidia katika shughuli ya kutathmini thamani ya mali iliyopatikana kazi ambayo hasi sasa haijafanyika isipokuwa makadirio ya dhana.

Baada ya kufanyika tathmini ya kitaalamu umiliki wa mali hizo utahamishiwa kwenye wizara ya fedha ya taifa hilo Mchambuzi  na mhariri mkuu wa gazeti la Al Tayyar la Sudan amesema kiwango cha ufisadi chini ya utawala uliopita  kilikuwa kikubwa mno na kilichotanuka.

AFP

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,419FollowersFollow
544,000SubscribersSubscribe

Latest Articles