24.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

SUDAN KUSINI NCHI HATARI ZAIDI KWA WAFANYAKAZI WA MISAADA

Sudan Kusini ndio nchi hatari zaidi yenye ukatili mkubwa kwa wafanyakazi kwenye mashirika ya misaada, utafiti wa Shirika lisilo la kiserikali la Humanitarian Outcomes umesema.

Utafiti huo unaonyesha kuwa, wafanyakazi wapatao 313 wa misaada wameathirika na mashambulizi makubwa hasa kwa mwaka jana.

Inaelezwa kuwa, hadi kufikia mwaka jana,  ni mwaka wa nne sasa tangu taifa hilo liingie kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe, na kusababisha uhasama wa kudumu dhidi ya wafanyakazi wa misaada.

“Ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo Sudani Kusini imeripotiwa kuwa sehemu ngumu kufikisha misaada katika vita hivi, na kutokujali mashambulizi yanayofanywa dhidi ya wafanyakazi wa misaada,” alisema Katibu Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norwegian Jan Egeland.

Hata hivyo, viongozi wa pande zote mbili za vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Kusini mwa Sudan wamesaini makubaliano ya kusitisha mapigano wiki iliyopita, wakitumaini kupunguza vurugu dhidi ya wananchi na wafanyakazi wa misaada.

Naye Geno Teofilo, Mkuu wa Mawasiliano na Ushauri Ukanda wa Afrika Mashariki na Yemen kwa NRC, amesema kama makubaliano ya amani yalivyosainiwa hivi karibuni, ikiwa migogoro yote itasimama, itachukua muda kuboresha nchi.

Aliongeza kuwa Sudan Kusini bado inakabiliwa na mgogoro mkuu wa chakula na hakuna fedha za kutosha za msaada, ambapo ilisababisha usambazaji wa chakula cha msaada kwa maelfu ya watu.

Vilevile, njaa inaweza kuendelea mwaka huu, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mwezi Januari na Shirika la Kimataifa la U.N. limekadiria zaidi ya watu milioni 7 watakuwa katika mgogoro mpaka kufikia nusu ya kwanza ya mwaka huu, na watoto milioni 1.3 chini ya umri wa miaka mitano watapatwa na utapiamlo.

Teofilo aliongeza kuwa, kwa taifa ambalo linasumbuliwa daima na vita na uhaba wa chakula, makubaliano ya amani huleta matumaini kwamba misaada ya kibinadamu itaweza kuendelea kufanya kazi bila vurugu kubwa katika siku zijazo.

“Mpango huu wa hivi karibuni wa amani ni hatua muhimu, kwenye safari ndefu ya amani na tunatarajia kuwa itasaidia kumaliza mgogoro huo pia ifahamike kuwa watu Sudan Kusini wanatamani amani,” amesema Teofilo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,051FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles