Suarez: Nipo hapa kuipa timu ubingwa

0
4410

luis-suarez-fc-barcelonaBARCELONA, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Barcelona, Luis Suarez, amesema kwamba yupo katika timu hiyo kwa ajili ya kuipa ubingwa.

Nyota huyo amekuwa na kipindi kizuri katika klabu hiyo kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao, ambapo juzi klabu hiyo ilishuka dimbani katika mchezo wa nusu fainali ya Copa del Ray dhidi ya Valencia, huku mchezaji huyo akiifungia timu hiyo mabao manne kati ya 7-0.

Katika mchezo huo, Suarez alionekana kuwapa wakati mgumu walinzi wa Valencia, huku mabao matatu yakiwekwa wavuni na bingwa wa Ballon d’Or, Lionel Messi.

“Nipo hapa kwa ajili ya kuisaidia timu yangu, ninaamini ninafanya hivyo kwa kuwa timu inafanya vizuri na ninatoa mchango wangu wa kufunga mabao.

“Mchezo wa jana (juzi), naweza kusema kuwa nimeonesha kiwango kizuri na kuwapa furaha mashabiki wangu baada ya kufunga mabao manne.

“Timu inacheza kwa ushirikiano mkubwa, hasa nikiwa na Messi na Neymar, najua Neymar alikosa penalti, lakini tulikuwa tayari kushirikiana ili aweze kupata bao ila bahati haikuwa yake,” alisema Suarez.

Mbali na kupachika mabao hayo kwenye michuano hiyo, Suarez amekuwa na kipindi kizuri katika michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania, ambapo hadi sasa ana jumla ya mabao 19 katika msimamo wa Ligi sawa na Cristiano Ronaldo.

Kocha wa Barcelona, Luis Enrique, amempa pole kocha wa Valencia, Gary Neville, kutokana na kichapo alichokipata kutoka kwa vijana wa Camp Nou.

“Timu yoyote ambayo itakutana na sisi ni jambo la kawaida kuondoka na kichapo, siyo tu kwa Neville, kwa kuwa ndio kazi yetu na lengo letu, kwa upande wangu sikuwa na lengo baya, lakini ilikuwa ni kazi yetu,” alisema Enrique.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here