24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Suarez ataviweza viatu vya Messi Ballon d’Or?

Lionel+Messi+Luis+Suarez+FC+Barcelona+v+Cordoba+dxAnXGK5F5Rl

ADAM MKWEPU NA MITANDAO,

MIEZI michache iliyopita nyota wa timu ya Barcelona, Lionel Messi, alikuwa mfalme wa dunia, lakini kwa sasa inaweza kuwa ngumu kurudia alichokifanya wakati huo ambapo alifanikiwa kuongeza idadi ya tuzo za uchezaji bora duniani na kufikia tano.

Kwa sasa kijiti hicho huenda akamuachia mchezaji mwenzake katika timu hiyo, Luiz Suarez, katika mbio hizo lakini je, nyota huyo ataweza kuvaa viatu vya Messi?

Kwa miaka sita mfululizo ilikuwa vigumu kusikia jina tofauti kati ya  Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika tuzo ya ufungaji bora wa mabao  ndani ya msimu mmoja.

Suarez amefanikiwa kuvunja rekodi hiyo kwa kushinda mabao 40 kwa mwaka kwa kuisaidia Barcelona kuchukua kwa mara ya pili mfululizo ubingwa wa Ligi Kuu Hispania.

Suarez, ambaye anaonekana kuwa na safari ndefu katika soka mwenyewe amejinadi kwamba anaweza kushinda taji hilo huku akijua wazi ugumu uliopo katika kufanikisha nia yake.

Miguu ya nyota huyo inatarajiwa kufanya makubwa katika ardhi ya Catalunya na kuwasaidia kunyakua ubingwa kwa mara nyingine msimu ujao.

Katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Suarez alionekana kuipa uhai timu hiyo.

Katika Ligi Kuu ya Hispania, La Liga, Suarez alifunga mabao 33 na kusaidia kupatikana mabao 15 huku Messi akifunga mabao 29 na kusaidia kupatikana mengine 16 wakati Ronaldo alifunga 27 na kusaidia kupatikana mabao nane.

Hata hivyo, ushindani mkubwa ataupata kutoka kwa Ronaldo ambaye msimu huu ana kila sababu ya kunyakua tuzo hiyo baada ya kulisaidia taifa lake kuibuka na ubingwa wa michuano ya Euro 2016 msimu huu huku akiwa tayari amechukua ubingwa wa Ligi ya Ulaya.

Kwa Messi inaonekana mambo kumwendea kombo baada ya kukosa kombe la Copa America kwa mara ya pili mfululizo likienda Chile.

Licha ya kuonekana kushindwa kufurukuta, lakini bado ubora wa Messi unabaki pale pale kwa kuwa ni mchezaji ambaye anatamani mafanikio.

Suarez anaamini kwamba hata kama Messi hatafanikiwa msimu huu lakini Ronaldo atabaki kuwa nafasi ya pili kwa ubora dhidi ya nyota huyo wa taifa la Argentina.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles