27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 7, 2023

Contact us: [email protected]

SUALA LA DAWA ZA KULEVYA KWA WASANII LIMECHANGANYA MASHABIKI

NA GRACE SHITUNDU- DAR ES SALAAM

TASNIA ya burudani imeingia katika kashfa nzito baada ya Alhamisi wiki hii Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutaja orodha ya majina ya watu mbalimbali wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Jambo lililogusa nyoyo za mashabiki wa burudani Tanzania ni pale yalipotajwa majina ya mastaa wa filamu na muziki ambao wanatuhumiwa kutumia dawa za kulevya na aliwataka jana saa tano asubuhi akutane nao Kituo Kikuu cha Polisi Kati kwa mahojiano.

Mastaa kama Wema Sepetu, Rachel, Babuu wa Kitaa, Mr Blue, Chid Benz, Dogo Hamidu, TID na wengine walitajwa kwenye orodha hiyo na kufanya habari hiyo ipokelewe kwa mshtuko na mitazamo tofauti kutoka kwa mashabiki huko mtaani mpaka kwenye mitandao ya kijamii.

Msanii kama Chid Benz hakushtua sana kwa sababu tayari alishajitangaza kuwa anatumia dawa za kulevya na mara kadhaa amepelekwa kwenye soba kwa ajili ya kupata matibabu ya kumsaidia kuacha matumizi hayo.

Ila hao wasanii wengine ndio wamewaweka njiapanda mashabiki kufuatia heshima yao, umaarufu wao na mashabiki wengi walionao, hapo ndipo maswali mengi yalipogonga kwenye vichwa vya mashabiki.

Unajua msanii ni kioo cha jamii, msanii ndiye anayeweza kutengeneza au kuibomoa jamii kutokana na watu wengi wanaomtazama. Kwa maana hiyo chochote anachokifanya au kinachosemwa juu yake kinaifikia jamii kwa uharaka zaidi.

Bila shaka tuhuma hizi zimeleta mkanganyiko kwa mashabiki, hakuna anayejua kipi kinaendelea kwenye uhalisia wa maisha yao. Haijulikani kwa sababu bado ni watuhumiwa hakuna uthibitisho.

Tatizo hili la dawa za kulevya kwa muda mrefu limekuwa likipoteza wasanii wengi ambao nyuma yao kulikuwa na familia zinazowategemea na mashabiki lakini leo hii hawana uwezo tena kisanaa.

Ikumbukwe kuwa hao ni watu maarufu ila nyuma yao kuna mamilioni ya vijana mashabiki ambao nao tayari ni waathirika wa dawa hizo hatari za kulevya.

Huu ni wakati wa mashabiki kutulia na kusubiri nini kitaendelea kwenye sakata hili lililoitikisa tasnia ya burudani wiki hii.

Nampongeza sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kwa hatua hii nadhani sasa tunaelekea kupunguza na hatimaye kumalizika kabisa tatizo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles