30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Stiegler’s Gorge sasa mwendo mdundo

AnnaPotinus, Dar es Salaam

Serikali ya Tanzania na Misri zimesaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Stiegler’s Gorge ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2,100 za umeme.

Mkataba huo umesainiwa leo Jumatano Desemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo baada ya kusaini mkataba huo uliokuwa kati ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Misri, Mostafa Madbouly, Watanzanaia wameombwa kuonesha ushirikiano wao kwa kuwa na mshikamano hadi hapo mradi huo utakapokamilika.

“Niwaombe wananchi wanaoishi kwenye vyanzo vya maji muunge mkono mradii huu kwa kutunza vyanzo vya maji, msichome miti hovyo na kwa bahati nzuri Wakuu wa Mikoa wote mko hapa,” amesema Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema mradi huo wa umeme wa Bonde la Mto Rufiji ulianza tangu kipindi cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, lakini kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo za kifedha nchi ilishindwa kutekelezajambo hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles