28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Steve Bruce kocha mpya Newcastle United

NEWCASLE, ENGLAND

KLABU ya Newcastle United imethibitisha kuwa Steve Bruce atakuwa meneja wao mpya katika mkataba wa miaka mitatu.

Newcastle ilimtangaza Bruce jana, baada ya kukubali kulipa fidia ya  fidia ya Euro milioni nne kwa klabu ya Sheffield.

Bruce mwenye umri wa miaka 58, hakuweza kuficha furaha yake, baada ya kuchukua nafasi ya Rafa Benitez aliyetimuliwa.

 “Ninafurahi na najivunia sana kuchaguliwa kuwa kocha mkuu wa Newcastle United.

 “Hii ni klabu yangu ya utotoni na ilikuwa klabu ya baba yangu, hivyo huu ni wakati maalum sana kwa ajili yangu na familia pia.

 “Kuna changamoto kubwa mbele yangu, lakini mimi na wasaidizi wangu tuko  tayari kupambana nayo.

“Tutapambana kuhakikisha tunawapa kila kitu mashabiki wetu ili waweze kujivunia timu yao,”alisema Bruce.

Bruce ataungana na makocha, Steve Agnew na Stephen Clemence huko Newcastle na wote watatu watasafiri kwenda China kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu mpya.

Mkurugenzi Mkuu wa Newcastle, Lee Charnley, alisema: “Steve ana upendo mkubwa kwa Newcastle United na tunafurahi sana kuwa na kocha mwenye uzoefu mkubwa na uhusiano na klabu na mji amejiunga na sisi.

“Steve anajua kile klabu hii inamaanisha kwa mashabiki na ataweka moyo wake na roho kuongoza kundi la wachezaji wenye vipaji kwa msaada wa uongozi wa klabu.

“Kazi ngumu kwa Steve na timu yake huanza mara moja na tutajitayarisha kikamilifu na changamoto ya msimu mpya wa Ligi Kuu.

“Napenda kumshukuru Ben Dawson, Neil Redfearn na wafanyakazi wetu wa matibabu na msaada kwa njia ambayo wamefanya kazi pamoja ili kusimamia mwanzo wa maandalizi yetu ya kabla ya msimu,”alisema Charnley.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles