StarTimes yazindua msimu mpya ‘Hello Mr Right’

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital 

Kampuni ya StarTimes, imezindua  msimu  wa tano wa kipindi cha ‘Hello Mr Right’ kinachotarajia kuanza kurushwa wikiendi hii.

Akizungumza na waandishi wa habari Leo Novemba 28,2023,  Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, David Malisa amesema kuwa msimu huu wa watashuhudia burudani iliyoboreshwa tofauti na misimu mingine iliyopita.

“Leo ndio tunaizindua rasmi msimu  tano wa Hello Mr Right Show, kuna mengi makubwa tumeboresha na kuongeza radha ambayo  kila mtazamaji atafurahia, ‘show’ hii itaruka kupitia chaneli ya ST Bongo kuanzia Jumamosi hii tarehe 02/12/2023 saa 3:00 usiku. 

Amesema watoto pia hawajaachwa nyuma kwani wameongeza chaneli nyingine ya watoto Kwa kuwa hiki ni kipindi ambacho shule zimefungwa. 

“Tumeongeza chaneli ya Boing kwa ajili ya watoto kuburudika wakiwa nyumbani chaneli hii inapatikana katika visimbuzi vyote cha dishi na Antena,” amesema.

Kwa upande wa muendeshaji wa kipindi hicho  Mc Garab, amesema kuwa msimu wa tano utakuwa pia na darasa la mahusiano na ushauri

” Kuna surprise nyingi ambazo tumeziweka ndani ya msimu wa 5 wa Hello Mr Right Show kutakuwa na elimu mbali mbali kuhusu afya, darasa kwa ajili ya mahusiano’Dating Booth’ ambapo watakuwa wanapewa ushauri  vitu vingi vinavyohusu mahusiano,” amesema.