24.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 8, 2021

Startimes yaunga mkono juhudi za Serikali kupambana na corona

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Star Media kupitia chapa yake ya StarTimes imeunga mkono juhudi za serikali katika kupamba na virusi vya Corona (Covid 19) kwa kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa huo.

Meneja uhusiano kwa Umma, Pendo Benson alisema kuwa kwasasa wameanza kurusha kipindi cha StarTimes Daily Covid-19 Report ikiwa ni sehemu ya kutimiza azama yao .

“StarTimes imeanza kurusha kipindi kinachotoa habari na taarifa muhimu kuhusu virusi vya Corona ikiwemo elimu ya namna ya kujikinga ,kupitia chaneli ya ST Swahili kila siku saa 3:45 usiku,na pia kupitia Application ya StarTimes ON kwenye simu janja,”alisema Pendo.

Alieleza kuwa lengo lao kubwa ni kuwahabarisha watu wa maeneo yote ya mijini na vijijini ili wajue namna ya kujikinga.

“Watu wamekua na wasiwasi mkubwa na maswali mengi kwa kupata habari zisizo sahihi kupitia mitandao ya kijamii,hii imepelekea kua na ugumu wa upatikanaji wa habari za uhakika,hivyo basi StarTimes itawahabarisha na kuwaelimisha kuhusiana na virusi vya Covid -19,”alibainisha.

Aidha aliwataka wananchi kuzingatia tahadhari zitolewazo na mamlaka husika ikiwemo wataalamu wa afya.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
168,538FollowersFollow
527,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles