Startimes yapewa tuzo ya Tacaids

0
686

Mwandishi wetu

Kampuni ya ving’amuzi ya Startimes imepata tuzo kutoka kwa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania kupitia Jukwaa la Bongo Star Search, kipindi kinachoruka ndani ya chaneli ya ST Swahili kinacholenga Kusaidia na kuelimisha vijana juu ya maambukizi ya Virusi vya ukimwi ambapo vijana ndio walengwa wakubwa.

Tuzo hiyo imetolewa leo katika Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza ambapo kampuni hiyo imeahidi kutajitahidi kadri ya uwezo wake kuchangia na kuisaidia Serikali kupambana na  vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Makamu wa Rais wa Kampuni, Carter alitoa shukrani zake za dhati na kukabidhi mchango wa Shmilioni tano kama mchango wao katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa ukimwi.

“Ni heshima kubwa sana kupokea tuzo ya Tacaids. Sisi Kampuni ya Star Media Tanzania tutajitahidi kwakadri ya uwezo wetu kusaidia Serikali kwa kuchangia kupiga vita maambuki ya Virusi vya Ukimwi Tanzania na kutokomeza kabisa ifikapo mwaka 2030,” amesema Carter.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here