33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

StarTimes yajivunia mafanikio

Mwandishi Wetu

Kampuni ya Ving’amuzi ya StarTimes imesema inajivunia mafanikio iliyoyapata ikiwamo kujitoa kwa jamii katika kutoa misaada mbalimbali.
Aidha, imesema hadi sasa imefanikiwa kutoa kipaumbele kwa jamii katika kuhakikisha inarudisha kile inachopata hasa katika kuunga mkono taasisi zisizo za kiserikali na sekta ya filamu Afrika.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatoa huduma kwa takribani watu milioni 30 katika nchi 37, ukuaji huu mkubwa umeifanya kampuni hiyo kuwa muendeshaji mkubwa wa runinga barani Afrika na pia katika kuhakikisha inaleta maudhui mazuri kwa wateja wake.


“Tangu tumeingia katika soko la Afrika mwaka 2018, StarTimes imejitahidi kufikia malengo yake ili kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata nafasi na uwezo wa kutazama Televisheni ya Kidigitali.


“Mwaka jana StarTimes ilifanikiwa kutoa mchango wake kwa jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo kuchangia Polisi vifaa vya michezo, vile vile ilichangia elimu katika kampeni ya Tokomeza Zero Kisarawe kiasi cha Sh milioni 10 katika kusaidia Serikali kwenye jitihada za kuhakikisha inatokomeza Zero.


“Aidha iliweza kutembelea kituo cha watoto yatima kitwacho Chawama kilichopo Sinza na kuwapatia msaada kiasi cha Sh milioni tatu na kudhamini tamasha la muziki la Wasafi Festival lililofanyika katika mikoa mitano na kumalizikia jijini Dar es salaam,” imesema taarifa hiyo.


Pamoja na mambo mengine, kampuni hiyo pia imefanikiwa kudhamini mashindano ya kusaka vipaji ‘Bongo Star Search’ ambayo yalikwenda vizuri na kuhitimishwa vizuri.


Kwa upande wa tuzo, taarifa hiyo imesema kampuni hiyo ilikabidhiwa tuzo kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) ambapo kampuni hiyo kwa kutambua mchango wao nao wakatoa Sh milioni tano ili kusaidia serikali katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles