29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Stars piga hao Guinea ya Ikweta

MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

TIMU ya Tanzania, Taifa Stars, leo saa 1:00 usiku itashuka kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na Guinea ya Ikweta ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kundi J kuwania kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021), zitakazofanyika Cameroon.

Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa kumbukumbu ya kutinga hatua ya makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022, zilizopangwa kufanyika nchini Qatar.

Timu hiyo ambayo ipo chini kocha Etienne Ndayiragije ilifanikiwa kuitoa Burundi kwa mikwaju ya penalti 3-0 baada ya timu kutoka sare bao 1-1 katika mchezo awali wa  marudiano uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Taifa.

Kabla ya matokeo hayo, timu hizo zilipata  sare kama hayo katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Bunjumbura nchini Burundi.

Pia, Taifa Stars itaingia uwanjani ikiwa imetoka kufuzu michuano ya Afrika kwa wachezaji wanacheza Ligi ya Ndani (CHAN), baada ya hivi karibuni kuifunga Sudan mabao 2-1 katika mchezo wa marudiano uliochezwa ugenini, ambapo kabla ya mchezo huo, Stars ilifungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa.

Akizungumzia mchezo huo, Ndayiragije alisema kikosi chake kipo tayari kwa mapambano ya kusaka ushindi wa kwanza nyumbani ili kujiweka vizuri katika mbio za kuwania nafasi ya kushiriki Afcon ijayo.

“Kila kitu kipo sawa kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Guinea ya Ikweta, tunafahamu umuhimu wa mchezo huu, ndiyo maana tumeweka msisitizo wa hali juu ili kile tulichopanga kiweze kutimia, tunajua kazi haitakuwa rahisi kupata matokeo hapa, lakini kwa uwezo wa Mungu na maandalizi tuliyofanya tutashida.

 “ Tutaanzia nyumbani hicho ni kitu muhimu zaidi kwetu, tuantaka kutumia faida ya kucheza nyumbani kujipatia pointi tatu muhimu, lazima tuhakikishe tunashinda mechi zote hapa ili kurahishisha mazingira, tuko tayari kujitolea kwa kadri ya uwezo wetu kuwapa Watanzania kile wanachokitaka, ,”alisema Ndayiragije.

Nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Samatta, alisema watahakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo ili kufuta mkosi walioanza nao mwaka 2017 kwa Lesotho.                                

Alisema safari hii hawako tayari kurudia makosa ya kuruhusu hata sare nyumbani , huku akieleza kuwa watahakikisha kila atakanyaga Taifa anakutana na kichapo.

 “Tunajua tuna mchezo mgumu, tumejipanga vilivyo na tuko tayari kuipambania nchi, wachezaji wote tumepewa maelekezo na benchi la ufundi kilichobaki ni kwenda kuyatekeleza uwanjani.

 “Tutahakikisha tunashinda, hatoturuhusu makosa tuliyofanya kwa Lesotho, lazima tutumie vizuri uwanja wetu wa nyumbani kupata pointi tatu kila mchezo, tulipata tabu kipindi kile kutokana na kushindwa kufanya vizuri hasa mchezo ule wa kwanza, ugenini ni ngumu kupata ushindi, hivyo lazima tushinde nyumbani,” alisema .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles