30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

STAILI YA TRUMP BURUDANI TUPU

NA AGATHA CHARLES,

WIKI iliyopita, Donald Trump (70), aliapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani na kufuatiwa na sherehe iliyofanyika katika majengo makuu ya Bunge la Congress, mjini Washington.

Katika hafla hiyo rangi zilizotawala kwa wahusika wakuu ilikuwa ni nyekundu, bluu, nyeupe na nyeusi.

Trump alivaa suti yenye koti refu kutoka lebo ya mavazi ya kiume ya Brioni chini ya kampuni ya Ufaransa iitwayo Kering.

Trump ambaye amekuwa mteja wa miaka mingi katika lebo hiyo, alivaa pia tai ndefu iliyovuka mkanda wa suruali ambayo inadaiwa kutengenezwa nchini China.

HAFUNGI KOTI

Hiyo ndiyo staili yake. Trump hana kawaida ya kufunga vishikizo vya koti lake. Hata siku ya kuapishwa muda wote koti lake lilikuwa wazi, iwe amekaa au amesima hali hiyo iliruhusu tai yake ndefu kuonekana ilikoishia.

Wachambuzi wa mitindo wanaeleza kuwa vishikizo vya koti vinapaswa kufungwa wakati wa kukaa na kufunguliwa unaposimama.

Kwa miaka mingi sasa Trump huvaa tai ndefu zaidi tofauti na ilivyokuwa miaka ya 1984 alipokuwa anavaa tai zinazoishia katikati ya mkanda wa suruali.

Moja ya sababu zinazotajwa ni kutokana na umbo lake ambalo akivaa tai ya kawaida inaweza isikae vyema tumboni.

Mmoja wa wachambuzi, Joseph Abboud, anasema Rais huyo alivutia kwa mavazi yake kwa kuwa alivaa rangi za bendera ya Marekani, kitamaduni zaidi kwani anapenda zaidi rangi nyeusi.

Angalau wakati wa hafla ya jioni, Trump alivaa suti nyeusi ya Tuxedo, shati jeupe pamoja na bow tai nyeusi.

MELANIA

Mara kadhaa nimeandika kuhusu mavazi ya Melania (46), yanayokwenda na wakati kwani hilo ndilo eneo lake hasa kwa kuwa aliwahi kuwa mwanamitindo.

Wakati wa kuapishwa mumewe, Melania alivaa gauni na kikoti cha rangi ya poda bluu kutoka kwa mbunifu Mmarekani, Ralph Lauren.

Nguo hiyo alimechisha na gloves pamoja na viatu, inashabihiana na ile ya mke wa Rais wa 35 wa taifa hilo, John F. Kennedy, Jacqueline ambayo nayo ilibuniwa na Ralph Lauren.

Mwaka 1961 wakati wa kuapishwa mumewe, Jacqueline alivaa nguo ya rangi kama ya Melania pamoja na gloves lakini aliongeza na kofia.

Wafuatiliaji wa mitindo wanatoa maoni kuwa huenda Melania aliamua kuiga rangi hiyo kutoka kwa mbunifu huyo ambaye amekuwa akiwavalisha baadhi ya wake wa marais wa nchi hiyo akiwemo, Hillary Clinton.

Katika hafla ya usiku ambayo pia wawili hao walicheza muziki pamoja, Melania alipendeza na gauni lake la ‘Off-the –shoulder’ rangi ya ivory kutoka kwa mbunifu Mfaransa.

USIYOYAJUA

Melania ni ‘first lady’ ni mke wa tatu wa Trump walifunga ndoa mwaka 2005.

Kabla yake, mwaka 1990 aliolewa Marla Maples mama wa Tiffany (22), ambaye alikuwa mtangazaji.

Katika mitandao mbalimbali ikiwemo Daily na USA today, inamwelezea Melania na Trump walikutana wakati mfanyabiashara huyo akiwa na mkewe wa kwanza, Czechoslovakian Ivana Zelnickova, mama wa watoto watatu, Ivanka (34), Eric (32) na kaka yao, Donald Trump Jr ambaye ana miaka (38), akiwa na tofauti ya miaka nane na mama yake wa kambo Melania.

Melania ni mama wa Barron (10) ni first lady wa kwanza kuzaliwa nchi ya Kikomunisti huko Yugoslavia ni wa pili pia kutoka ng’ambo baada ya Louisa Adams ambaye alikuwa mke wa Rais wa sita wa nchi hiyo, John Quincy.

Melania anazungumza lugha tano ikiwemo Kislovenia, Kiingereza, Kifaransa, Kiserbia na Kijerumani, harusi yake na Trump ilihudhuriwa na Bill Clinton na Hillary walikuwa miongoni mwa wageni 350.

Pamoja na sifa hizo, inadaiwa Melania ni first lady pekee aliyewahi kupiga picha za uchi katika kazi yake ya mitindo ikiwa ni miaka mitatu kabla hajakutana na Trump.

Tofauti yao na kina Obama

Moja ya vitu ambavyo Rais mstaafu wa nchi hiyo, Barack Obama, vilimpa umaarufu ni upendo wake kwa familia yake hususani mkewe ambao mara nyingi ulionekana hadharani.

Wawili hao, Michelle na Obama kama kawaida yao walionyesha upendo wakati wa mapokezi ya Rais mpya kwa mabusu ya hapa na pale.

Pamoja na kuwa vyama tofauti, wao walimpigia debe Hillary, lakini bado wote wawili walimshika kwa upendo Melania na kumwongoza lango la Ikulu.

Mtaalamu wa lugha za miili, Patti Wood, anasema wakati Trump na Melania wakiteremka kwenye gari Ikulu kujongea walipo Obama na mkewe, hawakuwa na mawasiliano huku Rais huyo akijijali mwenyewe kwa kumwacha mbali mkewe pasipo kumsubiri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles