21.2 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

SSRA YAWATOA HOFU WANACHAMA HIFADHI YA JAMII

Na NORA DAMIAN -DAR ES SALAAM          |          


MAMLAKA ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imewatoa hofu wanachama na wategemezi kuwa hakuna watakachopoteza baada ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hivi sasa Serikali iko katika mchakato wa kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii na tayari sheria ya kuanzisha mfuko mmoja wa watumishi wa umma (PSSF) ilishasainiwa tangu Februari mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA kwenye Maonyesho ya Vyuo Vikuu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam jana, Mkuu wa Mahusiano na Uhamasishaji wa SSRA, Sarah Kibonde, alisema wamefanya maandalizi ya kutosha na kwamba wanachama na wategemezi wataendelea kupokea mafao yao kama kawaida.

“Kila kitu kiko salama na michango yao iko salama, hivyo watu wasiwe na hofu kwa sababu kinachofanywa na Serikali ni kuboresha mafao ya wanachama na kuhakikisha yanawanufaisha sasa na baadaye,” alisema Kibonde.

Kuhusu Tanzania ya Viwanda, alisema wamelipa uzito suala hilo hasa kupitia sera ya uwekezaji ya mifuko ya hifadhi ya jamii, kwani wanatambua litasaidia kupanua wigo na kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii nchini.

Baadhi ya wananchi waliotembelea banda la SSRA, waliishauri mamlaka hiyo iendelee kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa hifadhi ya jamii.

Mmoja wa wananchi hao, Rosemary Joseph, alisema bado watu wengi hawana uelewa kuhusu masuala ya hifadhi ya jamii na umuhimu wa kujiunga na mifuko.

“Mimi natambua faida za hii mifuko hasa kwenye suala la matibabu inasaidia sana, unaweza kuugua ukajikuta huna fedha lakini ukiwa na bima ya afya una uhakika wa kupata matibabu,” alisema Joseph.

Idadi ya wanachama katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa sasa ni milioni 2.4.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,813FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles