24.6 C
Dar es Salaam
Saturday, September 7, 2024

Contact us: [email protected]

SportPesa kunogesha tamasha la Simba

Na Theresia Gasper -Dar es salaam

KLABU ya Simba imewajumuisha wadhamini wao SportPesa katika tamasha lao lililoboreshwa zaidi na kupewa jina la ‘SportPesa Simba Week’.

Tamasha hilo ambalo linatarajia kuanza kesho mwaka huu litakua linatimiza takribani miaka 10 tangu kuanzishwa.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, alisema katika wiki hiyo watafanya mambo mbalimbali ikiwemo kutangaza jezi zao mpya zitakazotumika msimu wa 2019/20.

“Katika tamasha letu ambalo tumeliita SportPesa Simba Week, tumeboresha vitu mbalimbali tofauti na miaka ya nyuma, tutaanzisha kadi mpya kwa mashabiki na wanachama ambayo itakuwa kama ya benki na itatumika katika kulipia kama unataka kwenda uwanjani kuangalia mechi,” alisema.

“Wachezaji wetu pia wanatarajia kuja Jumatano na baada ya hapo wataendelea na mazoezi lakini pia tutakuwa na siku ambao wataweza kupiga picha na mashabiki hususan watoto wadogo ambao wanawapenda wachezaji wao.”

Magori alisema kilele cha SportPesa Simba Week ni Agosti 6 mwaka huu katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Power Dynamos ya Zambia itakayochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 

Alisema tiketi za Platinum zitauzwa Shilingi laki moja huku zile za Platinum Plus zikiuzwa Sh. 150,000 ambapo mashabiki watapata hudumu za juu zaidi ikiwa ni pamoja na kukaa sehemu nzuri watakayoangalia mechi kiufasaha.

Magori aliongeza Agosti 4 mwaka huu watazindua wimbo wao mpya utakaokuwa unatumika katika tamasha hilo ikiwemo mashabiki wao kwenda kutoa damu.

“Wapinzani wetu Power Dynamos wanatarajiwa kuwasili Jumapili tayari kwa mchezo wetu wa Agosti 6 ambayo pia itakua maalumu kutambulisha wachezaji wetu,” alisema.

Magori alisema kabla ya mechi hiyo kutatanguliwa na mechi ya Simba Queens na kisha Simba B dhidi ya Fountain Gate.

Naye Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti Sport Pesa Tanzania, Abbas Tarimba, aliwapongeza Simba kwa shughuli nyingi za kimaendeleo ikiwemo kufikisha kipindi cha miaka 10 tangu waanzishe tamasha hilo.

“Tunashukuru kuwa na Simba pamoja katika wiki hii ya ‘SportPesa Simba Week’ kwasababu ni ni moja ya timu ambayo tumekuwa nayo kwa mafanikio mazuri ukizingatia tangu tuingie nao mkataba, wameweza kuchukua jumla ya Sh. million 200 baada ya kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo,” alisema.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kauli mbiu tamasha hilo ni ‘Iga ufe ‘This is next level’, 10 years Anniversary of Simba Week’.

“Tunawaomba mashabiki waanze kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu na wajitokeze hiyo siku kuujaza uwanja na kuwashuhudia wachezaji wetu wapya,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles