26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Spika: Zitto anadanganya

Spika wa Bunge Job Ndugai,amesema Mbunge wa Kigoma Mjini,Zitto Kabwe (ACT Wazalendo) anawadanganya wananchi.

Ndugai alisema uchambuzi wa ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), unaofanywa na Zitto unalenga
kuwaaminisha wananchi kwamba kila kilichomo kwenye ripoti hiyo ni cha kweli.

Alisema kwa upande wake humuungi mkono kwa kuwa ukweli wa ripoti hiyo hudhihirishwa na kamati mbili za Bunge ambazo ni kamati ya PAC na LAAC.

Spika Ndugai aliyasema hayo bungeni leo mchana muda mfupi kabla hajaahirisha Bunge hadi jioni.

Pamoja na hayo Spika alisema Zitto anatumia muda wake mwingi kuichambua ripoti hiyo kwa kuwa anataka awe Mwenyekiti wa Kamati ya PAC kinyemela.

Wakati huo huo huo Spika Ndugai aliwataka wabunge wawe wavumilivu kwa kutojadili mambo kabla muda wa kufanya hivyo haujafika kwa mujibu wa kanuni za Bunge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,631FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles