29.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai awaomba wabunge kuishauri Serikali

Na Brighiter Masaki, Dodoma

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungan wa Tanzania, Job Ndugai, amewataka wabunge kuchangia Mpango wa Taifa wa Maendeleo kwa kuishauri Serikali katika kufanya ununuzi wa ndege au isitishe hadi mambo yatakapo kuwa vizuri.

Ndugai ameyasema hayo leo Aprili 8, 2021 Bungeni Jijini Dodoma kabla ya kuchangia Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo (2021/22 hadi 2025/26) uliosomwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba.

Pia Spika Ndugai amesema Shirika la Ndege (ATCL) limepata hasara ya sh bilioni 60 na amewataka wabunge hao kushauri katika mpango mwingine wa ununuzi wa mabehewa kwa ajili ya uendeshaji wa reli ya kisasa (SGR) kama ni vyema yakanunuliwa na Serikali au ununuzi ukafanywa na wabia wa sekta binafsi.

Hata hivyo Ndugai amesema zipo nchi zinafanya uwekezaji wa miundombinu ya reli na suala la mabehewa linafanywa na wawekezaji binafsi na kuwaomba wabunge kutumia nafasi hiyo kuishauri Serikali na wasisubiri kukosoa wakati inapokosea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles