23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Spika Ndugai abariki viboko shuleni

Ramadhan Hassan

Spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema bila viboko shuleni mambo hayaendi vizuri.

Spika amesema hayo leo Alhamisi Januari 31, bungeni jijini Dodoma baada ya Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, kusema viboko vitaendelea kutumia shuleni.

Ole Nasha alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Zainab Katimba.

Katika swali lake Katimba alitaka kujua kama adhabu ya viboko inaongeza kiwango cha ufaulu.

Akijibu swali hilo, Ole Nasha amesema Serikali itaendelea kusisitiza matumizi sahihi ya adhabu kwa wanafunzi ili kuleta tija katika ufundishaji na ujifunzaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles