27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

SPIKA KIFICHO APONGEZA VITA DAWA ZA KULEVYA

Na MWANDISHI WETU


SPIKA Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho ameisifu serikali kwa juhudi zake za kupambana  na dawa za kulevya na  vitendo vya  rushwa vilivyokuwa vikishamiri nchini.

Hayo aliyasema mwishoni mwa wiki  kwenye mahafali ya nne ya Chuo  Kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika   Kawe Beach   Dar es  Salaam huku  akishuhudia  utolewaji wa  Shahada ya kwanza  ya  Udaktari wa Falsafa (PhD).

Alisema  ni jambo ambalo linatakiwa kuungwa mkono  na kila mmoja  Tanzania ibakie kuwa nchi safi bila dawa za kulevya. 

 Alisema kitendo cha kuendelea kutoa huduma ya elimu katika mazingira magumu, tena kwenye majengo ya kupanga, inaonyesha dhamira ya dhati  kuhusu namna ya kuendeleza na kukuza  elimu nchini.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Costa Mahalu alisema  wahitimu 499  wamefanikiwa kumaliza masomo yao kwenye fani mbalimbali, wanafunzi 45 ngazi ya cheti na Stashahada 47.

Wengine  ni  shahada 334, Shahada ya Uzamili 71 na Shahada ya Udamivu ni mmoja licha  ya uongozi wa chuo hicho kukabiliana   na changamoto  nyingi ndani ya miaka mitano.

Alisema anashukuru kwa kupata kibali cha  kufikia hatua hiyo ya kufanya mahafali, lakini bado kuna  changamoto ya majengo kwa kuwa  bado wapo kwenye  majengo ya kupanga.

Alisema iwapo serikali itabariki upo uhakika wa mahafali ya mwakani kufanyika  kwenye majengo ya chuo  yanayojengwa Kiromo  wilayani Bagamoyo.

 Alisema chuo kimekuwa na malengo  ya kuwasomesha wahitimu wa chuo  kwa kuwapeleka vyuo vingine katika shahada ya uzamivu   kupunguza tatizo la wahadhiri ambalo vyuo vingi nchini vinakabiliana nalo.

Awali, Kaimu Mkuu  wa Chuo hicho, Dk.William  Kudoja alisema  wanaendelea na utaratibu wa kuongeza kozi baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo ya chuo Bagamoyo.

Waliwaomba wadau ikiwamo serikali, kuhakikisha  wanasaidia kukamilisha   majengo  yao wenyewe na kuepuka  gharama kwenye majengo ya kupanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles