27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Array

Spika atangaza fursa mkutano wa CPA utakaofanyika nchini

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MKUTANO wa 50 wa Chama cha Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika (CPA), unatarajiwa kufanyika Agosti 30 visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na maspika 20 na wajumbe zaidi ya 400.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema kufanyika nchini mkutano huo, kutaambatana na fursa mbalimbali ikiwamo za kiuatalii.

Mkutano huo unatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein, na zaidi ya mataifa 14 yanatarajiwa kushiriki.

Ndugai alisema wageni mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo wakiwemo maspika wanachama, manaibu spika, wabunge, mabalozi kutoka nchi wanachama waliopo nchini na maspika kutoka mabara mengine.

Alisema hadi sasa maspika 20 kutoka nchi wanachama wamethibitisha kushiriki mkutano huo ikiwa ni pamoja na wabunge kutoka nchi hizo.

Ndugai alisema jumla ya washiriki 400 wanatarajiwa kushiriki mkutano huo na watautumia kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kuomba kibali kutoka kwa wajumbe wa mkutano huo kufanya uwekezaji jijini Dodoma wa kujenga hoteli ya nyota tano.

“Kule tuna kamfuko ketu, tutashawishi na tutaenda na agenda tujenge kitega uchumi hapa Dodoma na ni hoteli ya nyota tano maana tumekuwa tukikutana na changamoto ya Jiji la Dodoma kutokuwa na hoteli za nyota tano,” alisema.

Spika Ndugai aliwashauri wafanyabishara kuchangamkia  fursa ya mkutano huo.

“Hivyo naomba kuwashauri wafanyabiashara na Watanzania wenzangu kwa ujumla fursa hizi tunazozipata za kuaminiwa na mataifa mbalimbali tuzichangamkie. Ni fursa adhimu,” alisema.

Aidha alisema Bunge la Tanzania ni makini ndiyo sababu limeaminiwa na mkutano huo unafanyika hapa nchini.

“Naomba niseme Bunge letu ni makini na linaaminiwa na ndiyo maana vikao vingine vidogo vidogo vya kamati za hiki chama huwa mara nyingi vinafanyika hapa Tanzania. Hii kwetu ni heshima kubwa kwa kweli,” alisema Ndugai.

Katibu wa Bunge, Steven Kagaigai  alisema hadi sasa maandalizi yote ya mkutano huo yamekamilika na ameaahidi utafanyika kwa usalama wa hali ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles