Spika alirudisha Jimbo la Serengeti mikononi mwa NEC

0
2583

Mwandishi Wetu, DodomaSpika wa Bunge, Job Ndugai, amemuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa Jimbo la Serengeti liko wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano, hatua hiyo imekuja baada ya Spika Ndugai kupokea barua kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Marwa Ryoba ya aliyejiuzulu nafasi ya Ubunge na kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

“Spika ameandika barua hiyo kwa mujibu wa Kifungu 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Sura ya 343, iliyojadidiwa mwaka 2015) kinachoelekeza

kwamba, pale ambapo Mbunge, atajiuzulu, atafariki au ataacha kazi ya ubunge kwa sababu nyingine yoyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113 cha

Sheria hiyo, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha Ubunge kiko wazi,” imesema taarifa hiyo.

 

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here