28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

SOS yazikutanisha nchi nane kujadili hatma ya watoto

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wadau kutoka mataifa manane ya Afrika wanakutana jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kutafuta njia za kuwasaidia watoto wanaolelewa katika vituo vya malezi mbadala kumudu maisha wanapotoka kwenye vituo hivyo.

Mshiriki kutoka Zambia katika Mkutano Maalumu ulioandaliwa na Kijiji cha Watoto cha SOS, Clare Chilambo akizungumza na wanahabari wakati wa Mkutano huo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kandoni mwa mkutano huo, Mratibu wa Vijana kitaifa kutoka Kijiji cha Watoto cha SOS, Samson Anthony alisema mkutano huo unahusisha nchi 8 zinazoendesha vituo hivyo.

“Lengo ni kujadili maendeleo ya watoto waliopelewa katika vituo vyetu, kwa kuwa tumeona mara nyingi tumeona wanapotoka vituoni kwenda uraiani wanashindwa kumudu mazingira.

“Kwa hiyo tunaangalia namna ya kuwawezesha kuendana na jamii wanaporudi uraiani, ambapo tayari kwa Tanzania tumeshaunda mtandao maalum yangu Agosti mwaka jana,” alisema.

Alisema wanaendelea kubadilishana mawazo na kupeana uzoefu ambapo Zimbabwe ndiyo iliyofanikiwa vizuri katika suala hilo, hivyo nchi nyingine zinaendelea kujifunza kwao.

Anthony alisema nchi zote nane zinazoshiriki katika mkutano huo, bazo ni Kenya, Rwanda, Zambia, Tanzania, Afrika Kusini, Somalia na Ghana ziko katika hatua mbalimbali za maandalizi ya kuunda mtandao huo.

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Makao ya Watoto Mkoa wa Dar es Salaam, Evance Nyegete alisema wanahitaji kupata namna bora ya kuwasaidia watoto wanaolelewa vituoni kwa kuwa mwisho wa siku ni lazima warido katika maisha ya kawaida na waweze kujitegemea na kuishi vizuri kwenye jamii.

“Lengo ni kuangalia namna bora ya kuwasaidia vijana hawa kujitegemea. Tunaona badala ya kupungua, watoto hawa wanaongezeka kutokana na umaskini, malezi duni, migogoro ya familia na watoto wengine wameachwa bila ulinzi kutokana na mila na desturi.

Mwenyekiti wa Wamiliki wa Makao ya Watoto Mkoa wa Dar es Salaam, Evance Nyegete akizungumza na wanahabari wakati wa Mkutano maalumu wa kujadili hatma ya watoto wanaolelewa vituoni.

“Tunaona pia kutokana na majukumu na mahangaiko ya maisha wazazi wanawatunza tu badala ya kubakwa watoto, lakini pia wengi wanaoanzisha makao hawana elimu sahihi ya kuwatunza watoto, kwa hiyo vikao kama hivi vinatusaidia kuja na majawabu,” alisema.

Mshiriki kutoka Zambia, Clare Chilambo alisema kwa sasa wanaangalia namna ya namna ya kuwafanya watoto hao waweze kujikimu baada ya kutoka kwenye vituo vya malezi, ambapo wengi wamekiwa wakishindwa kumudu kujitegemea na kurudi kuomba kuendelea kusaidiwa vituoni.

Mmoja wa vijana aliyelelewa kwenye kituo cha Kijiji cha Watoto cha SOS, ambaye kwa sasa ni Mratibu wa Vijana wa mtandao wa Care Leavers Tanzania, Amani Amani alisema mtandao huo una lengo la kuwaunganisha vijana waliolelewa vituoni na ndugu zao, ili kuweza kujitegemea, mara watakapotoka kwenye vituo vya malezi.

“Tunaona Serikali imekuwa ikiandaa programu za kuwawezesha vijana kama ilivyo kwa Building a Better Tomorrow (BBT), tunaomba programu kama hizi ziangalie pia namna ya kuwachukua vijana wanaolelewa vituoni ili waweze kuwa na uhakika wa kujitegemea,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles