25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

SOMALIA YAPONGEZWA KWA MABADILIKO YA KIUSALAMA

Umoja wa Mataifa, Muungano wa Afrika, Muungano wa Ulaya, Serikali ya Uingereza na Serikali ya Marekani wamefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Waziri Mkuu wa Somalia, Hassan Ali Khaire kuwaeleza wadau hao wa kimataifa kuhusu mabadiliko katika sekta ya usalama nchini humo na mipango inayochukuliwa na serikali kuendelea kuimarisha hali ya usalama Somalia.

Taarifa iliyotolewa na mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM inasema jumuiya ya kimataifa imetiwa moyo na ari ya serikali ya shirikisho ya Somalia ya kutekeleza mabadiliko ya lazima ya kiusalama, kiuchumi na kisiasa na imehimiza msaada wake kwa ajili ya mabadiliko hayo.

UNSOM imesema jumuiya ya kimataifa inatarajia majadiliano zaidi wakati mikutano ya Benki ya Dunia na shirika la fedha duniani IMF, itakayofanyika mwezi April.

Pia wadau hao wamesema wanatarajia maamuzi muhimu kwa ajili ya msaada kwa mpango wa muungano wa Afrika nchini Somalia , AMISOM hasa ikijiandaa kukabidhi jukumu la ulinzi kwa Wizara ya ulinzi ya Somalia.

Jumuiya hiyo ya kimataifa imesema ina imani ya utekelezaji kikamilifu wa mabadiliko hayo nchini Somalia ambayo yatachangia kuleta utulivu na ustawi kwa watu wa Somalia na ukanda mzima.

Wamewachagiza wadau wote kusaidia na kuunga mkono juhudi za pamoja ili kuisaidia serikali ya Somalia kufikia azima ya mabadiliko hayo kupitia mchakato jumuishi wa majadiliano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles