25.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 29, 2021

Solskjaer yuko salama Man United

Manchester, England

BAADA ya timu ya Manchester United kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Burnley, Jumatano wiki hii, uongozi wa timu hiyo umeweka wazi bado una imani na kocha wao Ole Gunnar Solskjaer.

Kichapo hicho kilidhaniwa kingeweza kumuweka katika wakati mgumu kocha huyo huku mashabiki wakitumia mitandao ya kijamii kuutaka uongozi uachane na kocha huyo.

Kwa sasa Manchester United inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, ikiwa na jumla ya pointi 34 baada ya kucheza michezo 24. Hii ni mara ya kwanza kwa Manchester United kuwa na pointi chache kwenye Ligi hiyo baada ya miaka 30.

Mara ya mwisho kwa Manchester United kuwa na matokeo kama hayo ilikuwa msimu wa mwaka 1989-90, ambapo walikuwa na pointi 25 baada ya kucheza michezo 24 na msimu huo United ilimaliza nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi.

Baada ya kichapo hicho cha Jumatano, Solskjaer alikuwa anatajwa angekuwa kocha anayefuata kufungashiwa mabagi yake, lakini viongozi wamedai bado wanaamini kocha huyo anaweza kubadilisha mwenendo wa timu.

Mmiliki wa timu hiyo Glazers pamoja na makamu mwenyekiti Ed Woodward, walikutana na kuweka wazi hawawezi kumfukuza kwa sasa hata kama timu hiyo ipo kwenye hatari ya kushinda kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kocha huyo hadi sasa amepoteza jumla ya michezo 12 tangu achukue jukumu moja kwa moja la kuifundisha timu hiyo kutoka mikononi mwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jose Mourinho.

Mchezo unaofuata wa Ligi Kuu ambao Manchester United watashuka dimbani ni Jumamosi ijayo dhidi ya Wolves ambapo United watakuwa kwenye uwanja wa nyumbani Old Trafford.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,301FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles