27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Soko la madini lazinduliwa Kagera

Renatha Kipaka

NAIBU Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo ametoa mwezi mmoja  kwa Ofisa mMadini wa Mkoa wa Kagera, Lucas Mlekwa   kuwapatia leseni wachimbaji ambao wako tayari kutumia leseni zao.

 Agizo hilo alilitoa baada ya kusomewa taarifa ya madini mkoani hapa kuhusiana leseni ambazo hazitumiwi na wamiliki waliokwisha kuomba kwa muda mrefu.

 Alikuwa akizungumza na wachimbaji,wafanyabiashara wa madini hayo katika Kijiji cha Nyaruzumbura Kata Nyaruzbura  alipozindua soko  la madini wilayani Kyerwa.  

 Nyongo alisema  endapo kuna makampuni au mtu binfsi ameshindwa kuendeleza leseni zake apatiwe hati ya makosa na kurudisha leseni  wachimbaji wanaohitaji kutumia leseni hizo wapewe.

 “Ofisa madini natoa maelekezo endapo kuna kampuni au mtu binfsi ameshidwa kuendeleza apatiwe hati ya makosa na kurudisha leseni yake ndani ya mwezi mmoja,” alisema Nyongo.

 Alisema   watu wengne wanamiliki leseni ambazo hazifanyiwi kazi.

Naibu waziri alisema hao  ndiyo wanaoshusha kiwango cha uchimbaji hivyo  zifanyiwe kazi mara moja kama zamani  i kuongeza uchimbaji wa madini ikizingatiwa tayari kuna soko la uhakika.

 Alisema kwa kutambua umuhimu wa madini ya bati yanayopatikana mkoani Kagera pekee, Rais amefungua soko kwa ajiri ya kuzuia utoroshwaji wa wa madini hayo. 

Naibu waziri alisema utunzaji wa leseni bila kufanyia kazi ni kushidwa kufikia tija ya soko.

Alisema matarajio  ni kupata madini mengi   kuvutia wafanyabiashara kutoka nje kuja kwenye soko hilo.

Awal,i   Mlekwa alisema  serikali ilitoa leseni 248 za kuchimba mwaka 1998 kwa ajili ya wazawa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles