23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

SOFIA RICHIE, SCOTT DISICK MAMBO HADHARANI

LOS ANGELES, MAREKANI

HATIMAYE mwanamitindo maarufu nchini Marekani, Sofia Richie, ameamua kuanika uhusiano wake na Scott Disick.

Awali, Disick mwenye umri wa miaka 34, alikuwa anatoka na dada wa Kim Kardashian, Kourtney Kardashian, lakini kwa sasa ameamua kutoka na Sofia mwenye umri wa miaka 19, mtoto wa mkongwe wa muziki nchini humo, Lionel Richie.

Sofia na Disick wamekuwa wakionekana mara kwa mara miezi ya hivi karibuni, lakini juzi waliamua kuweka wazi kuwa wapo kwenye uhusiano.

Kupitia akaunti ya Instagram ya Disick, aliamua kuposti picha akiwa anamfungulia mlango wa gari mrembo huyo mara baada ya kumaliza kula chakula cha mchana mjini Los Angeles na kuandika ‘yupo chini ya uangalizi wangu’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles