26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

SNURA AWANG’ATA SIKIO MASTAA SIMBA

NA JESSCA NANGAWE


STAA wa Bongo    Fleva, Snura Mushi, amewang’ata sikio wachezaji wa timu ya Simba kuelekeza nguvu zao kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Snura ambaye ni shabiki mkubwa wa timu hiyo, ameeleza hisia zake kwa kikosi hicho baada ya     kushindwa kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Simba iliondolewa kwenye michuano hiyo na timu ya Al Masry ya Misri baada ya kutoka sare ya  2-2 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kushindwa kuifunga timu hiyo katika mchezo wa ugenini.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Snura aliwapa moyo wachezaji hao huku akiamini ubingwa ndio utawapunguzia machungu.

“Yale ni mashindano na lazima tukubaliane na matokeo, mimi kama shabiki wao mkubwa nimesikitika kushindwa kusonga mbele lakini nashukuru vijana walipigana kiume, kazi iliyobaki wanatakiwa kutusahaulisha machungu kwa kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu,”    alisema Snura.

Aliongeza kuwa kutokana na kiwango cha wachezaji wa Simba ni dhahiri ubingwa kwao hauzuiliki huku akiwataka kuongeza umakini kwa kuwa wapinzani wao nao wapo kwenye mbio hizo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles