23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

SMZ WAREKEBISHA SHERIA YA MTOTO

Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar,  Jaji Mshibe Ali Bakar

Na JUMA SALMIN-PEMBA

KATIBU wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar, Asma Hamid Jidawi,  amesema Serikali ipo mbioni kufanya marekebisha ya Sheria ya Ushahidi wa Mtoto namba 9 ya mwaka 2016.

Sheria hiyo  inampa nafasi mtoto kumtia hatiani mtuhumiwa aliyefanya vitendo vya udhalilishaji.

Hayo aliyasema hivi karibuni alipozungumza na wadau wa sheria kwenye mkutano uliofanyika   Micheweni.

Alisema awali suala la ushahidi wa mtoto lilikuwa tatizo katika kesi za udhalilishaji na ubakaji Visiwani Zanzibar.

Asma alisema mtoto alikuwa hana haki ya kutoa ushahidi unaoweza kumtia hatiani mtuhumiwa kutokana na kuhitaji ushahidi wa nyongeza katika kesi husika.

Kwa sasa sheria hiyo inakubali pia ushahidi wa  elektoniki, alisema .

Awali,   Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar,  Jaji Mshibe Ali Bakar, alisema sheria hiyo  imekwisha kupitishwa na Baraza la Wawakilishi na imezingatia hali za watu na mazingira kwa kuondoa mlolongo wa mashahidi katika kusimamisha kesi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles