27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

SMZ kuanzisha mfuko wa hija

Rais  wa  Zanzibar  na  Mwenyekiti  wa  baraza la  Mapindunzi, Dk. Ali  Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapindunzi, Dk. Ali Mohamed Shein.

Na MWANDISHI WETU,PEMBA

SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) iko mbioni kuanzisha mfuko wa hija  kuwawezesha Waislamu wasiokuwa na uwezo lakini wana nia ya kwenda kutekeleza ibada ya hija.

Katika hotuba  yake  ya  Baraza  la  Iddi jana, Rais  wa  Zanzibar  na  Mwenyekiti  wa  baraza la  Mapindunzi, Dk. Ali  Mohamed Shein  alisema  mfuko  huo  pia utasaidia  wastaafu  ambao wamekuwa  wakitumia  fedha  zao  za  kiinua  mgongo kwa  ajili  ya  kwenda  kutekeleza ibada  ya  hija     Makka,  Saudia Arabia.

Dk. Shein  aliyaeleza  hayo  katika  ukumbi  wa  Chuo  cha  Mafunzo  ya Amali Mkanyageni  Wilaya  ya  Mkoani,  Mkoa  wa  Kusini  Pemba  alipozungumza  na waumini  wa  dini ya kiislamu waliohudhuria   baraza  la  Iddi  ambalo  kitaifa limefanyika  kisiwani humo.

Ili kufanikisha suala hilo, Dk. Shein  alizitaka  taasisi  zinazojihusisha na kupeleka  mahujaji  kushirikiana  na  Serekali kupitia  Kitengo  cha  Wakfu  na  mali  amana   kuhakikisha waislamu wanaokwenda kufanya ibada ya hijja  wanakwenda  na  kurudi  salama.

Alisema     Sh  bilioni 16 .2  zimelipwa     kwa wastaafu 1,193 na kati  yao,  90 wamepewa  fursa  maalum  kwa  ajili ya kwenda  kutekeleza ibada  ya  hija  ambayo  ni  nguzo  mojawapo  katika nguzo  za  kiislamu.

“Ni vema taasisi zinazochughulika na usafirishaji wa mahujaji kuendelea kushirikiana na serikali kupitia kitengo cha wakfu na amali amana kuhakikisha mahujaji wanapata huduma  muhimu  wakati wote wanapotekeleza ibada hiyo,” alisema Dk. Shein.

Dk. Shein pia aliwaasa Waislamu kuendelea kudumisha amani ya nchi kwa kutii sheria ambayo ndiyo msingi katika kuleta mshikamano wa wananchi hivyo kufikia maendeleo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles