SMITH, JADEN WAFUNGUA KAMPUNI YA MAJI

0
794

NEW YORK, MAREKANI


STAA wa filamu nchini Marekani, Will Smith na mtoto wake Jaden, wametangaza kufungua kampuni ya kutengeneza maji inayojulikana kwa jina la ‘Just’

Hatua hiyo imefikia baada ya mtoto huyo kwenda shule na kupata elimu ya maji na mzingira, hivyo aliamua kukaa chini na baba yake na kisha kufikiria suala hilo la kuwa na kampuni yao ya kutengeneza maji.

“Hii ni kampuni ambayo inatokana na elimu ya mtoto wangu Jaden, kampuni hii haipo kwa ajili ya watu maarufu, lengo kubwa ni kuhakikisha kila mmoja anaweza kuyapata na kuyatumia maji hayo.

“Wazo la kampuni hii lilianza tangu mwaka 2015, lakini hatukuwa tayari kwa wakati huo kutokana na mwingiliano wa mambo, tunadhani huu ni wakati wa kuitangaza,” alisema Smith.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here