31.9 C
Dar es Salaam
Sunday, January 16, 2022

SmartLab yawakutanisha wamiliki wa kampuni, wawekezaji

Dar es Salaam, Tanzania


KATIKA kuwajengea uwezo waanzilishi wa kampuni mbalimbali, Jukwaa la Mwanzilishi kwa waanzilishi ‘ leo limefanya awamu ya tatu ya mikutano yake yenye lengo la kuwakutanisha wamiliki wa makampuni, wawekezaji na wadau mbalimbali.

Mkutano huo ni mfululizo wa mikutano inayoratibiwa na Kampuni ya SmartLab inayowaleta pamoja wavumbuzi mbalimbali na kujengeana uwezo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwanzilishi wa kampuni hiyo ya SmartLab, Edwin Bruno, alisema majadiliano katika jukwaa hilo hulenga kuibua mada mbalimbali ili kupata ufahamu wa jinsi ya kukuza kampuni mpya.

Bruno ambaye pia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Smart codes Limited alisema mojawapo ya changamoto inayowakabili waanzilishi wa kampuni nchini ni jinsi ya kukuza kiufanisi soko la kampuni husika.

“Mwanzilishi kwa Waanzilishi ni jukwaa kwa ajili ya kampuni mpya kukutana na wawekezaji, waanzilishi wenza na washirika.
Pia inawawezesha kuungana na kushirikiana wakati wa kubadilishana mawazo ya ubunifu kwa ajili ya kukua, kubadilisha mitazamo na kutengeneza ufumbuzi wa mambo mbalimbali kulingana na mazingira ya kitanzania na Afrika kwa ujumla.

Aliongeza “Kampuni mpya, wajasiriamali, wabunifu na wavumbuzi wa biashara za hapa nyumbani sasa wana sehemu moja ya kukutana na kufanya shuguli ambazo zitakutanisha na kukuza jumuiya za uvumbuzi zilizo tofauti na zenye vipaji hapa Tanzania na Afrika kwa ujumla kupitia Mwanzilishi kwa Waanzilishi”

Alisema Jukwaa la Mwanzilishi kwa Waanzilishi linatoa muungano wa muhimu ambao unawezesha wajasiriamali na kampuni mpya kujua mienendo mipya kwenye sekta ya uvumbuzi.

Aidha, Mkurugenzi wa Raha Liquid Telecom, Kumeil Abdulrasul, ambaye ni mdhamini mkuu wa jukwaa hilo, alisema ubunifu ndio hatima ya miaka na kizazi kijacho.

” Ndio maana Raha Liquid Telecom tunajivunia kuwa sehemu ya timu ambayo inataka kubadili hatima ya ubunifu, kampuni mpya na mazingira ya ubunifu Tanzania”.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,583FollowersFollow
530,000SubscribersSubscribe

Latest Articles