27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Small Planet yarudisha faida kwa jamii

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watoto 20 wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima kilichopo Tabata Msimbazi Kata ya Tabata wamepatiwa kadi za bima ya afya ili kuwawezesha kupata huduma bora.

Mkurugenzi wa Small Planet Bar, Andrew Msilanga (kushoto) akikabidhi jezi kwa Ofisa Elimu wa Jiji la Dar es Salaam, Mwalimu Mussa Ally kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zawadi. (Watatu kulia) ni Ofisa Mtendaji wa Kata ya Tabata, Revocatus Mapesa na Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata, Colle Senkondo.

Msaada huo umetolewa na Small Planet Bar iliyopo Tabata kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii ikiwa inasherehekea mwaka mmoja tangu ilipoanzishwa.

Mbali ya msaada huo uongozi wa baa hiyo pia umekarabati kisima cha maji katika kituo cha polisi Tabata, kupaka rangi ofisi ya mtendaji Tabata, kununua mashine ya kudurufu maandishi, kutengeneza meza katika Shule ya Sekondari Zawadi, kununua jezi za michezo na taulo za kike kwa wanafunzi 70.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya ya Tabata, Revocatus Mapesa, amesema uongozi wa baa hiyo baada ya kutimiza mwaka mmoja uliamua kurudisha faida kwa wanajamii wa Tabata kwa kutatua changamoto mbalimbali zilizopo.

Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Mwalimu Mussa Ally, akipokea meza 68 kutoka kwa Mkurugenzi wa Small Planet Bar, Andrew Msilanga kwa ajili ya Shule ya Sekondari Zawadi iliyopo Tabata.

“Walikuja ofisini wakatuuliza changamoto na tulipoziainisha wakaweza kufanya kwa sehemu kama mnavyoona, kutoa ni moyo si kila mtu anajaliwa kutoa hivyo tunapofanikiwa ni muhimu tukumbuke tulipotoka,” amesema Mapesa.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mwalimu Mussa Ally, ameipongeza baa hiyo kwa kuunga mkono jitihada za serikali ambayo imedhamiria kuleta elimu bora kwa kila Mtanzania.

“Tabata kuna wadau wengi na wenye uwezo lakini wewe umeguswa kwa kuona kwamba kuna haja ya kufanya kitu katika shule yetu tunashukuru sana,” amesema Mwalimu Ally.

Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi Tabata, Collo Senkondo, amekemea vitendo vya ukatili vinavyofanyika kwenye jamii na kuwataka wanafunzi kutoa taarifa katika vituo vya polisi pindi wanapofanyiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles