SL Savage kutoka Oman kuileta ‘Good Day’

0
965

MUSCAT, OMAN

KUNDI la muziki wa kizazi kipya linalofanya vyema nchini Oman, SL Savage, limewaomba mashabiki zake kukaa mkao wa kuburudika na ngoma yao mpya, Good Day.

Akizungumza na MTANZANIA jana, mmoja ya wasanii wanaounda kundi hilo, Lil Aziz alisema ngoma hiyo itatoka rasmi siku ya kesho kwenye mitandao (music platforms) mbalimbali duniani hivyo mashabiki wajiandae kuipakua na kuisikiliza.

“Baada ya kufanya vizuri na wimbo wetu Copy You, sasa SL Savage tunakuja na ngoma nyingine ya klabu ambayo itatoka Ijumaa hii, audio na video itapatikana kwenye chaneli yetu ya YouTube pia Spotify, Apple Music, iTunes, Deezer, Google Play na Anghami,” alisema Aziz.

Kundi hilo lililoanza mapema mwaka huu likiundwa na wasanii wakali wa kuimba kama Nas G, Aziz na Loca Boy na limeshafanikiwa kuachia nyimbo kadhaa zilizofanya vyema ndani na nje ya Oman.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here