31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

SITA WAKAMATWA KWA MAUAJI YA WAZIRI BURUNDI

BUNJUMBURA, BURUNDI


emmanuel-niyonkuruMAMLAKA za Burundi zimekamata watu sita wanaohusishwa na mauaji ya Waziri wa Mazingira, mwendesha mashitaka alisema hapa juzi.

Waziri huyo wa Maji, Mazingira na Mipango, Emmanuel Niyonkuru (54) alipigwa risasi na kufa wakati wa usiku wa kuamkia mwaka mpya, yakiwa mauaji ya mtu wa hadhi ya juu zaidi tangu mgogoro wa kisiasa wa Burundi uanze karibu miaka mwili liyopita.

Ijapokuwa polisi walikuwa wepesi kuyahusisha mauaji hayo na siasa, lakini kiini chake bado hakijajulikana.

Mwendesha Mashitaka Mkuu, Sylvestre Nyandwi aliwaambia wanahabari kuwa waziri huyo alipigwa risasi kichwani wakati akirudi nyumbani mjini hapa.

“Baada ya tukio hili baya, uchunguzi ulianza mara moja na washukiwa sita wamekamatwa, wakiwamo wanaume wanne na wanawake wawili,” alisema.

Nyandwi alisema uchunguzi bado unaendelea na hakubainisha utambulisho wa waliokamatwa au malengo ya mauaji.

Niyonkuru ni waziri wa kwanza kuuawa lakini waandamizi wengine wamelengwa na mashambulizi tangu mgogoro uibuke wakati Rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu April 2015.

Jenerali Adolphe Nshimirimana, anayehesabiwa kuwa mtu wa karibu wa Nkurunziza aliuawa Agosti 2015. Karibu mwaka mmoja taungu waziri wa zamanio na msemaji wa serikalim Hafsa Mossi auawe na watu wenye silaha akiwa katika gari lake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles