Sita wajitosa kumrithi Fatma Karume TLS

ANDREW MSECHU – dar es salaam

MAWAKILI sita wamejitosa kuwania nafasi ya urais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Aprili 6, huku mawakili zaidi ya 4,583 wanatarajiwa kushiriki.

Mkutano huo utafanyika wakati Rais anayemaliza muda wake, Fatma Karume akieleza msimamo wake kuwa hatagombea tena nafasi hiyo, hivyo kutoa mwanya kwa wagombea wengine.

Awali, Fatma alieleza nia yake ya kugombea tena nafasi hiyo lakini baadaye alibadili nia hiyo.

Fatma alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Lissu ambaye aliwania na kuteuliwa kuwa Rais wa TLS kwenye mkutano wa Machi 2017, ambao ulikipa umaarufu chama hicho.

Lakini Lissu aliongoza kwa miezi sita tu, baada ya shambulio la risasi lililotokea Septemba mwaka huo akiwa bungeni mjini Dodoma.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya simu jana, Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uchaguzi wa TLS, Tom Bahame Nyanduga alisema hadi sasa wapo waliojitokeza na majina yao kupitishwa katika nafasi za juu.

“Waliojitokeza miongoni mwao ni mawakili sita ambao tayari wamejitokeza na wamepitishwa kuwania nafasi ya urais wa TLS katika uchaguzi huo,” alisema.

Alisema nafasi zinazowaniwa na kupigiwa kura katika ngazi mbalimbali ni kuanzia nafasi ya rais, makamu wake, mweka hazina, wajumbe wa baraza la uongozi na wajumbe wa ngazi zote za kanda katika kanda mbalimbali za TLS zilizowekwa kwa mgawanyo wa majukumu ya kimahakama.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uchaguzi ya TLS na kuthibitishwa na Mtendaji Mkuu wa chama hicho, Kaleb Gamaya, iliwataja wagombea hao kuwa ni Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira (Leat), Dk. Rugemeleza Nshala na aliyewahi kuwa rais wa chama hicho, John Seka.

Wengine ni mawakili Godfrey Wasonga, Gaspar Mwanalyeka, Godwin Ngwilimi na Charles Tumaini.

Katika nafasi ya makamu wa rais, waliojitokeza na kupitishwa na kamati hiyo ni mawakili Mpale Mpoki na Neema Massame, wakati katika nafasi ya mtunza hazina waliojitokeza na kupitishwa ni Hussein Mtembwa na Aziza Msangi.

Awali Nyanduga aliliambia gazeti hili kuwa wakati wakisubiri mkutano mkuu wa Arusha, kuanzia jana wanaendelea na semina maalumu kwa ajili ya uchaguzi na taratibu za uchaguzi za TLS katika ngazi za kanda hadi watakapokamilisha Machi 30.

Semina hizo zinaambatana na uchaguzi wa viongozi wa kanda, kabla ya kujumuika pamoja katika Uchaguzi Mkuu wa Arusha utakaotoa viongozi wa ngazi za juu, ambao ni rais, makamu wake, mweka hazina na wajumbe wa Baraza la Uongozi la TLS.

Alizitaja kanda hizo kuwa ni Dodoma, Morogoro, Iringa, Mbeya, Mtwara, Kagera, Shinyanga, Tanga, Mwanza, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Tabora, Arusha na Ruvuma.

Taarifa katika tovuti ya TLS inaonesha kuwa tayari kuna mawakili wanachama 4,583 ambao wana haki ya kupiga kura katika uchaguzi huo.

Mkutano huo utafanyika wakati Rais anayemaliza muda wake, Fatma akieleza msimamo wake kuwa hatagombea tena nafasi hiyo, hivyo kutoa mwanya kwa wagombea wengine.

Awali, Fatma alieleza nia yake ya kugombea tena nafasi hiyo lakini baadaye alibadili nia hiyo.

Fatma alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Lissu ambaye aliwania na kuteuliwa kuwa Rais wa TLS kwenye mkutano wa Machi 2017, ambao ulikipa umaarufu chama hicho.

Lakini Lissu aliongoza kwa miezi sita tu, baada ya shambulio la risasi lililotokea Septemba mwaka huo akiwa bungeni mjini Dodoma.

WAJUMBE

Pia wapo mawakili 21 waliojitokeza kuwania nafasi za wajumbe wa Baraza la Uongozi na kupitishwa ambao ni Harold Sungusia, Jebra Kambole, Paul Kaunda, Tike Mwambipile, Maria Pengo, Matojo Cosatta na Anjelina Nashon.

Wengine ni Edwin Alon, Atranus Method, Musa Kassim, Stephen Mwakibolwa, Jocob Mugendi, Nmbute Akaro, Elias Machibya, Deus Nyabir, Costantine Mutalemwa, Baraka Mbwilo, Edmund Ngemela, Magdalena Sylister, Leocard Kipengele na Armond Swenya.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here