23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Sirro: uhalifu nchini umepungua kwa asilimia 24

Mwandishi Wetu, Dodoma

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema ametoa takwimu za matukio ya uhalifu nchini ambapo amesema kwa ujumla yamepungua kwa asilimia 24.9.

IGP Sirro ametoa takwimu hizo leo Ijumaa Novemba 22, jijini Dodoma katika uzinduzi wa ujenzi wa nyumba 118 za polisi zinazojengwa jijini humo eneo la Nzuguni.

“Hali ya uhalifu nchini kwa sasa imepungua sana licha ya changamoto ya matukio machache ya kihalifu lakini ambayo hata hivyo yameendelea kudhibitiwa kwa nguvu kwa ushirikiano wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama.

Takwimu za uhalifu makosa ya jinai katika kipindi cha miaka minne ya utawala wako, makosa makubwa ya jinai kwa ujumla wake yamepungua kwa asilimia 24.9, lakini makosa ya ungang’anyi wa kutumia nguvu yamepungua kwa asilimia 54.2, kwa makosa ya usalama barabarani kwa asilimia 69.4 kwa takwimu hizo tangu uingie madarakani uhalifu umepungua sana,” amesema.

Aidha, IGP Sirro amesema kushuka kwa uhalifu ni matunda ya mchango mkubwa wa Rais Magufuli katika kuhakikisha watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama wanapata mafunzo, vifaa, motisha na mahitaji mengine muhimu.

“Hali hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake majukumu yake na ndiyo hayo yamechangia kupungua kwa uhalifu.

“Mheshimiwa rais na amiri Jeshi Mkuu, nikuhakikishie hata uchaguzi ulioko mbele yetu utafanyika salama jeshi la polisi tumejipanga vizuri pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalama,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles